• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

" Ni marufuku makundi ya Pikipiki kuchangisha michango isiyokuwa na tija kwa wanachama wake" Dkt .Phillis Nyimbi

Posted on: November 21st, 2019

Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt. Phillis Nyimbi amepiga marufuku tabia ya vituo vya pikipiki kulazimisha watu kujiunga na vikundi vyao kwa kuwalazimisha kujiunga na vikundi hivyo kwa gharama kubwa.

Akitoa katazo hilo katika kata ya Kishili, mkuu wa Wilaya ameonya vikundi vyote vya pikipiki maarufu kama bodaboda kuacha tabia ya kutafuta pesa kwa njia zisizo halali na badala yake kufuata kasi ya serikali ya awamu ya tano inayosisitiza watu wote kujituma na kufanya kazi bila kubughudhiwa na mtu ama kikundi chochote cha watu.

Mheshimiwa Nyimbi alitoa katazo hili baada ya kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Lushinge Deus kulalamika mbele ya mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kishili tarehe 21 Disemba  ambapo kijana huyo alisema kikundi cha waendesha bodaboda wa Kishili kimemlazimisha kuchangia shilingi milioni moja ili kujiunga na kituo chao kama mwanachama wa kituo chao.

Alisema "nimepata pikipiki ya mkataba lakini baada ya kulipa mkataba na kubakiza shilingi laki saba,nilikwenda kijiwe cha Kishili ili niendelee na shughuli ya kuendesha pikipiki lakini chakushangaza nilipofika kijiweni uongozi wa kijiwe uliamuru nifungiwe minyororo pikipiki yangu na nilipokataa kulipa gharama hiyo walinipiga marufuku kuendesha pikipiki hiyo Kishili na kama ntaendesha watanichomea pikipiki yangu"

Kwa kuzingatia maelekezo ya serikali ya awamu ya tano inayotaka wananchi wa hali ya chini kujishughulisha bila kusumbuliwa, mkuu wa Wilaya aliwataka viongozi wa kijiwe hicho kufika ofisi yake Ijumaa tarehe 22 Disemba 2019 wakiwa na vielelezo vyote vya kisheria ikiwa ni pamoja na ripoti za fedha, katiba na viambatanisho vingine vinavyoruhusu ukusanyaji huo wa fedha kufanyika.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana yuko katika ziara za kawaida za kikazi katika Wilaya yake akifanya mikutano ya hadhara katika kata zote za wilaya yake akisikiliza kero, malalamiko na ushuri kutoka kwa wananchi.


Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA March 03, 2023
  • AJIRA ZA SENSA ZA MUDA KWA MWAKA 2022 May 05, 2022
  • Tangazo la kazi za muda May 25, 2022
  • Tangazo la kazi za muda May 25, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Chanjo ya polio kuanza kutolewa

    November 29, 2022
  • MKUU WA WILAYA NA WADAU WA MAZINGIRA KUING'ARISHA MYAMAGANA

    September 29, 2022
  • MKUU WA WILAYA NA WADAU WA MAZINGIRA KUING'ARISHA MYAMAGANA

    September 29, 2022
  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza yaridhishwa na mpangilio wa ujenzi unaoendelea wa soko kuu la kisasa jijini Mwanza.

    September 01, 2022
  • Tazama Zote

Video

Kiapo cha wakuu wa wilaya wapya wa Mkoa wa Mwanza
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi
  • Zabuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • Matokeo ya Kidato cha Sita
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0768520195

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.