Mkuu waMkoa wa mwanza ataka wote waliohusika kwenye udanganyifu wa Mitihani kuchukuliwa hatua
Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe.John VK Mongella ameyasema hayo leo kwenye Kikao kazi elekezi alichokiitisha kwenye Ukumbi Mkubwa wa Jiji la Mwanza leo. Kikao kazi hicho kilijumuisha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa,Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Nyamagana, Wakuu wa Idara na Vitengo vya Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa Shule na Walimu wakuu wa Shule za Msingi.
Mhe.Mongella amesema wamiliki wa Shule,Wakuu wa Shule na Baadhi ya walimu ndiyo wahusika wakuu wa kuiba mitihani wakiwa na lengo la kufurahisha wazazi wengi ili waaminike na kusajili watoto wengi katika shule hizo.
Mhe.Mongella amewataka wamiliki wa shule wenye tabia ya kuiba mitihani waache kwa kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kuvuliwa nyadhifa zao na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Naye Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Dkt.Phillis Nyimbi alisema waliokamatwa kwa kuiba mitihani inaonekana walianza muda mrefu kwa kuwa za mwizi 40 ndio maana wamekamatwa.
“Tumesikitishwa sana wilaya yetu kutiwa doa la wizi wa mitihani na baadhi ya watu wachache wasio waadilifu licha ya wilaya yetu kujitahidi kufanya mambo ya kuleta maendeleo” alisema Dkt.Nyimbi
Hata hivyo Mhe.Mongella amewataka Polisi na TAKUKURU,kuwakamata wahusika wote wakati wakisubiria hatua zingine za kisheria kufuata.
Barabara ya Balewa
Sanduku la Posta: 1333,Mwanza
Simu: +255 28 250 1375
Simu ya Kiganjani: 0755741738
Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz
Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.