• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Mwanza City Council
Mwanza City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Mwanza

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Orodha ya Viongozi Waliopita
      • Wenyeviti wa Halmashauri
      • Wakurugenzi
      • Wakuu wa Wilaya
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Kilimo na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Uchumi, Mipango na Ufuatiliaji
      • Mazingira na Usafi
      • Fedha na Biashara
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mifugo na Uvuvi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mipango Miji na Mazingira
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA,Habari na Uhusiano
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria na Usalama
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya uwekezaji
    • Vivutio vya utalii
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Usafi wa mazingira na uhifadhi wa taka ngumu
    • Leseni
    • Kilimo
    • Mifugo na Uvuvi
    • Maji
  • Baraza la Madiwani
    • Orodha ya madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
    • Ratiba ya vikao
    • Mihtasari ya vikao vya baraza
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • TASAF
    • Mfuko wa Jimbo
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Waraka
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Video
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio Yajayo
    • Magazine

Afya

HUDUMA TUNAZOZITOA:

1. Utoaji wa huduma za Chanjo kwa watoto na wajawazito

Idara imepokea dawa za chanjo zifuatazo toka Mkoani kwa kipindi cha 2015 hadi 2016 Chanjo ya BC,chanjo ya Penta valent dozi, Chanjo ya Surua/Rubella, Chanjo ya bOpv Chanjo ya Pepopunda dozi (TTv), Chanjo ya PCv13,Chanjo ya Rotarix, Mabomba ya sindano 0.05ml, Mabomba ya sindano 0.5ml, Makasha maalumu ya (safety boxes)

Kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma za chanjo kutoka vituo 30 kwa mwaka 2015 hadi vituo 35 kwa mwaka 2016. Pia Kuendelea kuimarisha utoaji wa chanjo kutoka aslimia 100 kwa mwaka 2015 hadi asilimia 106 kwa 2016 kwa chanjo ya Penta valent 

Kuendelea kutoa huduma ya chanjo ya mkoba kwenye maeneo yasiyo na huduma za chanjo karibu, vituo vya Mahina, Igoma, Sahwa, Mkolani na Nyegezi Fumagila na Shadi.

 

2. UPATIKANAJI NA USAMBAZAJI WA MADAWA NA VIFAA TIBA KATIKA HOSPITALI, VITUO VYA AFYA NA ZAHANATI         2015/2016

Dawa muhimu (tracer medicines) zilipatikana kwa kiwango cha asilimia themanini na moja (85 %) katika vituo vya kutolea huduma za afya (15) Hospitali 1, vituo vya afya 2 na zahanati 12.vinavyomilikiwa na Halmashauri. Pia vituo vyote vilipata mgawo wa dawa za serikali kutoka MSD na kusambazwa.

Upatikanaji wa damu salama ni jumla ya lita 853 za mls 450 zilizopatikana ambayo ni sawa na asilimia 25% kati ya malengo ya lita 3400 kwa miezi 8.

Udhibiti wa magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele kwa watoto wa shule za msingi wenye umri wa miaka 5 hadi 15 ambapo walengwa walikuwa 88,323 kati ya hao wanafunzi wa kike ni 45,267 wanafunziwa kiume ni 42,362. Jumla walIopata dawa za minyoo ya tumbo ni 86,237 ni sawa na asilimia 91.6 na walioata dawa za kichocho ni 86,127 sawa na aslimia 91.5%

3. UDHIBITI WA MAGONJWA YA MALARIA PAMOJA NA UTOAJI WA HUDUMA ZA TIBA 

Wagonjwa waliopimwa malaria 47,138, waliopimwa kwa kutumia mRDT ni 11,767 na BS 35371 Mama wajawazito walipimwa malaria 4911 kati yao 345 waligundulka na malaria Jumla ya akinamama wajawazito 9668 walipewa dawa za SP kukinga watoto walioko tumboni dhidi ya Malaria ,akinamama wajawazito 1142 pamaoja na watoto 844 walipewa vyandarua vyenye viuatilivfu vya muda mrefu kwa ajili ya kujikinga na malaria.

  • Idara imefanikiwa kugawa vyandarua kwa wanafunzi wa shule za msingi jumla ya vyandarua 19,800 katika shule zote za msingi.
  • Kufanya ukarabati wa vituo 13 vya kutolea huduma za afya kwa kutumia fedha za matokeo makubwa sasa kwa vituo vya afya 2,zahanati 11

4. UHAMASISHAJI WA JAMII KUJIUNGA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF/TIKKA

  • Kuhamasiha kaya,Taasisi za srikali na zisizo za serikali pamoja na shule za sekondari kujiunga na mfuko wa afya ya jamii kumeongezeka kutoka wanachama hai 688 kwa mwaka 2015 hadi kufikia 1035 kwa mwaka 2016, na pia kuhamasisha na kushirikisha wanufaika wa mfuko wa TASAF kujiunga na mfuko hadi sasa tunajumla ya wanufaika toka TASAF 435.
  • Kuundwa kwa Bodi ya Huduma za Afya ya Halmashauri ya Jiji ,kamati za afya za vituo 15, na kamati 18 za afya za kata na pia kufungua akaunti za kila kituo katika benki ya NMB Mwanza.

5. UDHIBITI WA UGONJWA WA UKIMWI.

        Kwa mwaka 2015/2016 mpango wa upimaji wa hiari umefanyika na kupima watu 49,086 kati ya hao wanaume ni 21,803,na                   wanawake27,283, kati ya hao walioonekana na maabukizi ni 3,973 wakike 2478 na wakiume 1,495

        Kwa kupitia upimaji unaoanzishwa na mtoa huduma wamepimwa watu 3,3215 kati yao 14681 ni wanaume na 18534 ni                          wanawake, waliopata maabukizi ni 2357 na kati yao 897 wanaume na 1460 wakike.

 

6. USIMAMIZI WA SHUGHULI ZA USTAWI WA JAMII

        Tumetengeneza vitambulisho vya wazee 5872 na kugawiwa ,Mashauri 239 yaliendeshwa kwa wanandoa wenye migogoro katika         familia zao, watoto kesi 213 zimetolewa hukumu na kesi 26 bado zinaendelea , wazazi waliokuwa hawatoi matunzo wamewapatia       watoto 246 wao matunzo yenye thamani ya Tsh 18,593,450 kwa njia ya kuandikishana ofisini ,Jumla ya watoto wa wanaoishi                 mitaani 1314 walifahamika ,watoto 179 wameondolewa na kuunganishwa na familia zao, Jumla ya kesi za watoto zipatazo 239             zimesikilizwa mahakamani kati ya hizo, jumla ya kesi 37 za watoto zilifunguliwa , kati ya hizo kesi 27 za ubakaji wa watoto,                     zilihukumia, kesi 6 watoto walifanya makosa, kesi 4 watoto kupewa ujauzito.

7. USIMAMIZI WA USAFI WA MAZINGIRA

Kiwango cha kaya zenye vyoo bora kimeongezeka toka 49% hadi 53% hii imetokana na kufanyika kwa kampeni ya usafi wa mazingira katika kata za Buhongwa, Lwanhima,Mkolani,Nyegezi,Luchelele,abatini,Igoma ,na Kishili.

Uhamasishaji wa jamii ulifanyika katika masuala yafuatayo -unawaji wa mikono mara kwa mara baada ya kutoka chooni,Katika maeneo yanayouza vyakula kama vile Hotel,Migahawa,na mama lishe /Baba lishe wateja kunawa mikono kwa maji safi na sabuni

Kutoa elimu ya afya kwa jamii katika kata zote 18 na mitaa 175 na pia kudhibiti milipuko ya magojwa ya kuambukizwa .


Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA March 03, 2023
  • AJIRA ZA SENSA ZA MUDA KWA MWAKA 2022 May 05, 2022
  • Tangazo la kazi za muda May 25, 2022
  • Tangazo la kazi za muda May 25, 2022
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Chanjo ya polio kuanza kutolewa

    November 29, 2022
  • MKUU WA WILAYA NA WADAU WA MAZINGIRA KUING'ARISHA MYAMAGANA

    September 29, 2022
  • MKUU WA WILAYA NA WADAU WA MAZINGIRA KUING'ARISHA MYAMAGANA

    September 29, 2022
  • Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza yaridhishwa na mpangilio wa ujenzi unaoendelea wa soko kuu la kisasa jijini Mwanza.

    September 01, 2022
  • Tazama Zote

Video

Kiapo cha wakuu wa wilaya wapya wa Mkoa wa Mwanza
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fomu Mbalimbali
  • Kuhusu Sisi
  • Zabuni

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Vibali Kusafiri nje ya Nchi
  • Matokeo ya Kidato cha Sita
  • Utumishi
  • TAMISEMI
  • Idara Kuu ya Takwimu(NBS)

Watembeleaji

world map hits counter

Idadi ya wageni

freevisitorcounters's Website

Ramani Elekezi

Wasiliana Nasi

    Barabara ya Balewa

    Sanduku la Posta: 1333,Mwanza

    Simu: +255 28 250 1375

    Simu ya Kiganjani: 0768520195

    Barua Pepe: cd@mwanzacc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2017 Mwanza City Council . All rights reserved.